Saturday, April 18, 2015

AZAM FC WAICHAPA GOLI 2-1 KAGERA SUGAR

Posted By: kj - 7:27 PM

Share

& Comment

Azam FC hii leo wamefanikiwa kuondoa jinamizi la sare baada ya leo kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam complex.

Katika mchezo huo Azam Fc waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 40 kupitia kwa Franky Domayo na kuipeleka Azam FC mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0

Katika kipindi cha Kagera sugar walifanikiwa kusawazisha goli hilo katika dakika ya 54 kupitia kwa Babu Ally.

Alikuwa Gaudency Mwaikimba aliyeihakikishia Azam Fc pointi tatu katika dakika za mwisho wa mchezo kwa kuiandikia Azam FC goli la pili na kuendelea kuihakikishia Azam FC nafasi ya pili ambapo watapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michezo ya kimataifa hapo mwakani.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.