Tuesday, April 7, 2015

MBEYA CITY USONI MWA AZAM FC KESHO, BOLUE KUREJEA

Posted By: kj - 11:36 AM

Share

& Comment

Kesho mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Azam FC watakuwa katika uwanja wa Azam Complex kuwakabili Mbeya city katika muendelezo wa ligi kuu ya Tanzania bara, ambapo azam FC wako katika nafasi ya pili wakiwa nyuma kwa pointi 4.

Mchezo huo wa kesho utakuwa mchezo wa 4 kwa Azam FC kukutana na MBeya city ambapo katika michezo mitatu iliyopita Azam FC wamepata ushindi katika michezo miwili na kutoa sare mchezo mmoja.

Mchezo huo wa kesho utakuwa mchezo wa 4 kwa kocha George Best Nsimbe ambaye teyari ameongoza Azam Fc katika michezo mitatu na kufanikiwa kuppata ushindi wa goli 1-0 katika kila mchezo/

Baada ya kukosekana uwanjani katika michezo mitatu iliyopita kiungo Kipre Bolue anataaji kurejea kikosi kesho kama kocha atampatia nafasi ya kuvaa jezi ya Azam FC hapo kesho.

Azam FC wataendelea kukosa huduma ya kiungo Salum Aboubakari katika mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu yake ya kukosa michezo mitatu ya ligi kuu ya vodacom.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.