Wednesday, April 8, 2015

AZAM FC WABANWA NA MBEYA CITY

Posted By: kj - 6:21 PM

Share

& Comment

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya vodacom Azam FC wamejiweka katika mazingira magumu ya kutetea ubingwa wao baada ya leo kwenda sare ya kufungana goli 1-1 na Mbeya city.

Katika mchezo waleo ambao Azam FC walikuwa wanawakosa mshambuliaji Didier Kavumbagu na Kipre Tchechesambamba na beki Aggrey Morice, walikuwa wenyeji wa Mbeya city katika uwanja wa Azam complexs.

Katika mchezo wa leo ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko wakiwa bado hawajafanikiwa kuona nyavu za wapinzani wao.

Azam FC walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Kipre Bolue katika dakika ya 61 kabla ya Mbeya city kusawazisha kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Rafael Daudi na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana goli moja moja.

Kwa mujibu wa matokeo hayo ya leo Azam FC wamefikisha point 37 wakinyuma kwa pointi 6 dhidi ya yanga yenye pointi 43 katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom.

MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM

RnTimuPWDLFAGdPts
1YANGA20134336112543
2Azam FC19107226131337
3SIMBA SC2198427151235
4KAGERA SUGAR217771920-128
5MGAMBO SHOOTING208391719-227
6RUVU SHOOTING216871418-426
7MBEYA CITY2151061618-225
8JKT RUVU216691620-424
9NDANDA FC216691824-624
10STAND UNITED206681723-624
11Coastal Union225981423-924
12MTIBWA SUGAR205871921-223
13POLISI MORO214981321-821
14T. PRISONS2031161420-620

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.