Wednesday, May 6, 2015

AZAM HAOO, KIMATAIFA KWA MARA YA 4 MFULULIZO, WAIPONGEZA YANGA KWA UBINGWA KWA KUWAPA KICHAPO

Posted By: Unknown - 7:56 PM

Share

& Comment

Ni Azam na Yanga tena kwa mara ya tatu mfululizo katika michuano inayoandaliwa na CAF mwakani, baada ya leo Azam FC kupata ushindi wa goli 2-1 mbele ya mabingwa Yanga, katika mchezo uliochezwa katika mvua ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kabla ya mchezo huo wachezaji wa Azam FC walijipanga katika mlango wa kutokea katika vyumba vya kubadilishia nguo, kwa ajili ya kuipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Yanga walifanikiwa kupata goli katika dakika ya 11 kupitia kwa Adrey Countinho kwa mpira wa adhabu nnje ya kidogo ya eneo la hatari.

Baada ya dakika moja kiuongo chipukizi Bryson Raphaeli alifanya alichokifanya chipukizi mwenzake Mudathir Yahya katika mchezo dhidi ya Simba SC, kwa kuisazawazishia Azam FC, akitumia vyema pasi ya Franky Domayo.

Kutokana na mvua kunyesha kulipunguza umakini katika safu ya ushambuliaji kutokana maji yaliyokuwa yametuama katika vieneo mbalimbali ya uwanja na kupelekea Azam FC na yanga kupoteza nafasi kadhaa za wazi za kufunga.

Goli la pili la Azam Fc lilipatikana katika dakika ya 76 kupitia kwa Aggrey Morice na kuamsha shangwa katika uwanja wa Taifa kwa mashabiki waliojitokeza uwanjani.

Kwa mtokeo hayo ya goli 2-1 Azam FC wamefikisha pointi 48 ambazo simba sc hawawezi kuzifikia, na Azam FC kujihakikshia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.

Kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Taifa bendera na jezi za wapinzani wawili, Azam na Yanga walikaa pamoja bila kujali utofauti wa vilabu wanay]vyo shangilia.

Azam FC leo: Mwadini Ally, Himid Mao, Gadiel Michael, Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Mudathir Yahya, Brison Raphael/Bocco, Frank Domayo, Gaudence Mwaikimba/Kavumbagu, Kipre Tchetche na Brian Majwega.  

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.