Sunday, May 3, 2015

SIMBA WACHELEWESHA HATMA YA AZAM KIMATAIFA

Posted By: kj - 10:23 PM

Share

& Comment


Simba SC wameichelewesha Azam FC kujiakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani baada ya leo Simba SC kuifunga Azam FC goli 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa..

Katika mchezo huo uliochezwa huku muda mwingi wa mchezo mvua ikinyesha, Mabingwa wa msimu uliopita Azam FC waliuanza mchezo kwa kasi, na kufanikiwa kutengeneza nafasi ambazo walishindwa kuzitumia.

Mchezo huo ulichezwa zaidi kwenye eneo la kati ya uwanja huku Azam FC wakionekana kutawala eneo hilo katika nusu ya kwanza ya mchezo kabla ya kiuongo Salum Aboubakari 'Sure Boy' kuzawadiwa kadi nyekundu.

Kutoka kwa Salum Aboubakari kuliipa Simba SC nguvu ya kushambulia, na kutawala mchezo na kupelekea kocha George Nsimbi kumtoa Franky Domayo na nafasi yake kuchukuliwa na Bryson Raphaeli katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kufanya mabadiliko ya kumpumzisha Pascal Wawa aliyepata jeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Mudathiru Yahya, mabadiliko yaliyopelekea Shomari Kapombe kuamia katika nafasi ya ulinzi wa kati, huku Himid Mao akisogea katika nafasi ya ulinzi wa kulia.

Katika kipindi hicho Simba SC waliuwanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya 48 Ibrahim Ajibu aliiandikia Simba SC goli la kuongoza, kwa kichwa akiunga krosi ya Hassani Kessi.

Kuingia kwa goli hilo kulizidi kuipa uimara Simba SC na kuifanya Azam FC kuwa nyuma muda mwingi na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza.

Ilikuwa dakika ya 57, Mudathir Yahya aliisawazishia Azam FC goli, kwa ustadi wa hali juu, akiunga krosi ya Kipre Tcheche na kuirudisha mchezoni Azam FC.

Kuingia kwa goli hilo kuliendeleza mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa Simba SC, ambapo kama Kipre Tcheche, Kavumbagu na Majegwa wangekuwa makini wangeipatia Azam FC goli.

Alikuwa Ramadhani Singano aliyeipa ushindi Simba SC katika dakika ya 74, na kupelekea mchezo kumalizika kwa simba kuibuka na ushindi wa goli 2-1 na kufikisha pointi 44 huku Azam FC wakiwa na pointi 45.

Azam FC inahitaji pointi tatu katika michezo miwili iliyosalia kujiakikishia nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho mwakani, ambapo siku ya jumatano watakuwa na kibarua mbele ya yanga, kabla ya jumamosi kuhitimisha na Mgambo shooting.

Azam FC leo: Aishi Manula, Gardiel Michael, Shomari Kapombe, Aggrey Morice, Pascal Wawa/Mudathir Yahya, Himid Mao, Kipre Tcheche, Franky Domayo/Braison Raphael, Didier Kavumbagu/John Bocco, Salum Aboubakri, Brian Majegwa

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.