Wednesday, July 1, 2015

AZAM FC KUNDI MOJA NA KCCA KAGAME CUP

Posted By: kj - 3:04 PM

Share

& Comment

Makamu bingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam FC watakutana kwa mara ya pili katika mwaka huu na KCC ya Uganda katika michuano ya kombe la Kagame baada ya kukutana katika hatua ya makundi ya kombe la Mapinduzi lililofanyika mapema mwaka huu visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu ya makundi yaliyotangazwa hii leo, Azam FC watakuwa katika kundi moja na KCC kama ilivyokuwa katika kombe la mapinduzi mapema mwaka huu ambapo mchezo ulimalizika kwa sare.

Azam FC nnje ya KCCA vilevile katika kundi lao linahusisha Malakia na Adama City, ambapo michuano hiyo inataraji kuanza katikati ya mwezi huu katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.


MAKUNDI CECAFA KAGAME CUP:

KUNDI A
Yanga ( Tanzania)
Gor Mahia ( Kenya)
Khartoum ( Sudan)
Telecom ( Djibout)
KMKM ( Zanzibar )


KUNDI B
APR( Rwanda)
Al Shandy ( Sudan)
LLB ( Burundi)
Elman ( Somalia)

KUNDI C
Azam (Tanzania)
Malakia ( South Sudan)
KCC ( Uganda)
Adama City ( Ethiopia)


0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.