Thursday, July 2, 2015

AZAM FC YAICHAPA RANGERS GOLI 4, KIMWAGA AKIREJEA NA GOLI

Posted By: kj - 2:41 PM

Share

& Comment

Kikosi cha Azam FC kimeifanyia Friends Rangers kwa kuifunga mabao 4-2, mchezo uliochezwa leo Uwanja wa Azam Complex.

Joseph Kimwaga majeruhi wa muda mrefu aliyefanyiwa upasuaji mchini Afrika Kusini, alicheza mechi yake ya kwanza leo na kuipatia Azam bao la kufungia kalamu ya mabao hayo dakika ya 83 kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Mrundi Didier Kavumbagu.

Katika mchezo huo uliokuwa na kasi kutokana na namna Friends kuwa na wachezaji maarufu kama Haruna Moshi 'Boban', Stephano Mwasyika na Yusuph Mgwao walivyoupania ushindi.

Lakini pamoja na juhudi zao, Azam waliwazidi nguvu na kuwachapa mabao hayo ambayo la kwanza lilifungwa na Farid Mussa dk 20 pasi iliyotoka kwa Kelvin Friday.

Hadi kipindi cha kwanza kinaisha Azam FC iliyocheza mfumo wa 4-3-3 matokeo yalikuwa 1-1.

Aishi Manula,
Sebo - Mwantika - Aggrey - Gardiel,
Himid -  Brison Raphael -  Salum Abubakar,
Farid Mussa – Kavumbagu - Kavin Friday

Kipindi cha pili Azam FC ilifanya mabadiliko kadhaa ambapo alitoka David Mwantika na nafasi yake kuchukuliwa na Ismail Adam Gambo, Brison Raphael alimpisha Kipre Bolou, SSebo alimpisha Rymond, na Farid Mussa alimpisha Joseph kimwaga.

Salum Abubakar alikuwa nyota wa mchezo wa leo kwa kucheza soka la hali ya juu na kungara kiwanjani. Labda alikuwa akifurahia kurejea kwa kocha wake kipenzi Stewart Hall.

Kelvin aliifungia Azam bao la pili dakika 47 na la tatu lilifungwa na Mrundi Didier Kavumbagu dakika 62 kutokana na kazi nzuri ya Salum Aboubakary 'Sure Boy'.

Baada ya mchezo huo ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Azam akiwemo Makamu Mwenyekiti, Nassor Idrissa na msemaji wa timu, Jafar Idd, kocha wa Azam, Stewart Hall alisema, vijana wake wamejitahidi na wamecheza kwa kufuata maelekezo aliyowapa.

"Huu ni mwanzo lakini wamejitahidi sana kwa sababu kuelewa kitu kipya wanachojifunza sasa inahitaji muda. Ulikuwa mchezo mzuri kwa sababu kuna muda walicheza kwa kufuata maelekezo na wakati mwingine walijisahau, kidogokidogo tunakwenda,"alisema Stewart.

"Nilikuwa na timu yenye wachezaji 14 tu, lakini mambo yamekwenda vizuri."


Fiends ambayo ilikuwa chini ya kocha wake, Hery Mzozo, ilipata mabao yake kupitia kwa Ally Kaijage dakika ya 16 na Clif Antony Buyoya dakika ya 68.

Kikosi cha Azam FC

1. Aishi Salum, 2. Abdallah Kheri/Raymond Ngingila, 3. Gadier Michael, 4. David Mwantika, 5. Aggrey Morris, 6 Himid Mao, 7. Farid Mussa/ Kimwaga, 8. Sure Boy, 9. Kavumbagu, 10. Bryson Rapfael/Kipre Bolou & 11. Kelvin Friday. 

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.