Thursday, July 23, 2015

BOCCO: LENGO NI KUIPA TAJI LA KWANZA AZAM

Posted By: kj - 10:48 AM

Share

& Comment

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco amesema safari bado ni ndefu kuipa timu hiyo taji la kwanza la michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame. 

Bocco ameng’ara kwenye michuano hii ambapo amefunga mabao katika mechi zote mbili ilizocheza timu yake.

Azam sasa imefikisha pointi sita baada ya kushinda mechi mbili za kwanza dhidi ya KCCA ya Uganda (bao 1-0) na Malakia ya Sudan (mabao 2-0) na hivyo kujiweka vizuri kwenye kufuzu robo fainali.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bocco alisema lengo kubwa ni kuipa Azam taji la kwanza wa Kagame ingawa safari ya kufanya hivyo bado ndefu.

“Tumeshinda mechi mbili, lakini unajua wapinzani wetu nao wanataka kushinda, ili sisi tufike mbali ni lazima tujitahidi kushinda kila mechi na hapo tutatimiza lengo letu ya kutwaa ubingwa wa Kagame,” alisema Bocco.

Azam inawania kutwaa taji kwenye michuano hiyo inayofanyika nchini kama ilivyofanya mwaka 2012 ambapo ilifika fainali na kushindwa kutwaa taji mbele ya Yanga baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0.

Chanzo: Habari Leo

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.