
Azam FC leo imeshinda goli mbili bila katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la Kagame.

Azam FC ikiendelea kutumia mfumo wake wa 3-5-2 ikiwa na mabadiliko manne toka mchezo wa kwanza dhidi ya KCCA, ambapo Gardiel Michael alichukuwa nafasi ya Erasto Nyoni, Abdallah Kheri alichukuwa nafasi ya Said Morad, Jean Baptiste Mugerenzi (Migi) akichukuwa nafsai ya Himid Mao na Ame Ally akichukuwa nafasi ya Dider Kavumbagu.
Hii leo Azam Fc ilitawala vilivyo eneo la kati na kutengeneza nafasi kadhaa za kupata goli lakini wakafanikiwa kutumia nafasi mbili tu.
Alikuwa John Raphael Bocco aliyeandikia Azam FC goli la kwanza katika dakika ya 26 kwa mpira wa adhabu aliopiga moja kwa moja na kutinga nyavuni.
Goli hilo lilidumu kipindi chote cha kwanza huku katika kipindi cha pili Azam FC walianza na mabadiliko mawili ambapo alitoka Amme Ally na Gardiel Michael na nafasi zao kujazwa na Kipre Tcheche na Faridi Mussa Maliki.
Katiika dakika ya 50 Kiprew Tcheche alimalizia vyema kazi nzuri ya Shomari Kapombe na kuiandikia Azam FC goli la pili na kuipelekea Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Kwa ushindi wa leo Azam FC wamefikisha pointi 6 wakiwa wamnefuinga magoli matatu wakiwa bado hawaja ruhusu nyavu zao kuguswa.
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment