Monday, July 20, 2015

HALL: AELEZEA KWANINI ALITUMIA VIUNGO WENGI JANA

Posted By: kj - 3:39 PM

Share

& Comment

Kocha Stewart Hall aliwaanzisha viungo wengi na kucheza soka la kujihami na kushambulia kwa kutumia mipira mirefu.

Akizungumzia mbinu zake, Hall alisema alilazimika kutumia mbinu hiyo kwa sababu wachezaji wake wengi bado hawapo fiti.

“Tupo katika kipindi cha maandalizi ya mwanzo wa msimu, wachezaji wangu Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu na Ramadhani Singano bado hawajawa fiti kwa asilimia mia, lakini naamini tutafika fainali.” alisema Hall

Hall aliongeza kuwa timu inayomtisha zaidi ni Gor Mahia kwa sababu wamekuja wakati ligi ya Kenya inaendelea hivyo wachezaji wao wapo fiti.

Chanzo: Mwananchi

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.