Saturday, August 22, 2015

AZAM WAPOTEZA NGAO YA JAMII, RIKODI YA CLEAN SHEET YA ENDELEA

Posted By: kj - 7:35 PM

Share

& Comment

Kiungo chipukizi Farid Mussa Malik akiwa kazini leo Taifa
Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC leo wameendelea na rikodi yao ya kucheza mchezo 13 bila ya nyavu zao kuguswa, japo wameoteza kwa mikwaju ya penati 8-7 kwa yanga SC, ukiwa mchezo wa kwanza kwa kocha Stewart John Hall kupoteza toka arejee katika kikosi cha Azam FC.

Azam FC waliuwanza mchezo kwa kasi na kupelekea safu ya kiungo ya yanga kupoteza mipira ovyo na kucheza faulo zisizo na maana, kabla ya wao kuakaa saa baada ya dakika 15 za mchezo.

Katika kipindi cha kwanza yanga walitumia zaidi mipira mirefu na kila wakijaribu kupiga mipira mifupi ilikuwa ina ishia kwa viungo wa Azam FC.

Kama Kipre Tcheche na John Bocco wangekuwa makini wangeipeleka Azam FC mapumziko wakiwa mbele kwa goli 3 baada ya kupoteza nafasi 3 za kufunga kwa mashuti yao kuokolewa na kipa wa yanga Ally Mustafa Bathez.

Hukosefu wa utulivu vilevile uliwagharimu yanga katika kipindi hicho cha kwanza kupitia kwa Saimon Msuva na Donald Ngoma ambao katika nyakati tofauti nao walipoteza nafasi na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya bila kufungana.

Mchezo ulirejea kwa kasi ile ile katika kipindi cha pili huku dakika 10 za mwanzo ikichezwa zaidi mipira ya juu kwa kila upande.

Yanga walimpumzisha Said Juma na nafasi yake ikachukuliwa na Haruna Niyonzima na kupelekea Yanga kuimarika sehemu ya kati na kocha Stewart Hall kuamua kumpumzisha Mudathir Yahya na nafasi yake ikachuku8liwa na Jean Mugereneza (Migi).

Mabadiliko hayo yaliwafanya yanga kutawala mpira huku azam wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza ambapo amanusura Azam FC waandike goli kupitia John Bocco baada ya kushindwa kuunga pasi ya Farid Mussa Maliki na kuplekea dakika 90 kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Baada ya dakika 90 kumalizika mikwaju ya penati ilichukuwa hatima na yanga wakapata penati nane na kupoteza penati moja huku azam FC wakipata penati 7 na kupoteza penati 2.

Waliokosa penati ni Nadir Haroub Cannavaro kwa upande wa yanga, Pascal Wawa na Ame Ally Zungu kwa upande wa Azam FC.

Huku Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Amisi Tambwe, Andrey Countinho, Geofrey Mwashiuya, Kamusoko, Mbuyu Twite na Kelvin Yondan wakipata penati kwa upande wa Yanga.

Wakati Kipre Tcheche, John Bocco, Himid Mao, Aggrey Morice, Jean Mugereneza 'Migi', Erasto Nyonin na Shomari Kapombe walipata kwa upande wa Azam FC.

Kikosi cha Azam FC leo: Aishi Manula, Shomar Kapombe, Aggrey Morice, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Himid Mao Mkami, Franky Domayo/Ame Ally, Farid Mussa Malik, John Bocco, Kipre Tcheche na Mudathir Yahya/Jean Mugereneza (Migi).

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.