Saturday, August 15, 2015

HIMID: LAZIMKA YANGA WAKAE

Posted By: kj - 7:19 PM

Share

& Comment

Nahodha msaidizi wa mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, Himid Mao Mkami amefunguka na kusema kuwa wataichapa Yanga SC kwa mara nyingine watakapokutana katika mchezo wa Ngao ya Jamii. Timu hizo mbili ( Azam FC Na Yanga) zilikutana katika hatua ya Robo fainali ya michuano ya Kagame mwezi uliopita na Azam wakaibuka na ushindi wa mikwaju ya penalty.

Akizungumza kutokea Zanzibar walipoweka kambi ya kujindaa na msimu mpya, Himid amesema kuwa upinzani wa siku za karibuni baina ya klabu hizo mbili ni kutokana na ubora wa klabu hizo kwa sasa. Katika mahojiano haya niliyofanya na kiungo huyo amesisitiza ni lazima waishe Yanga ili kutwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa kufanya hivyo mara tatu mfululizo.

www.shaffihdauda.co.tz; Hongera kwa ushindi wa Kagame Cup

HIMID; Asante sana, Mungu anasaidia

www.shaffihdauda.co.tz; Nini siri ya mafanikio kama timu?

HIMID; Siri ya mafanikio ni timu nzima, tunashinda kama timu ikitokea kufungwa tunafungwa kama timu. Lengo la timu ni kushinda na siyo kufungwa ndiyo mana tunapata matokeo mazuri.

www.shaffihdauda.co.tz; Ubingwa wa Kagame umewaongea kitu gani ukiachana na mafanikio ya ubingwa?

HIMID; Umetuomgezea kombe moja zaidi kwenye kabati la makombe pale Chamazi lakini,  ni kombe lenye heshma kubwa kwa ukanda wetu, pia ni njia nzuri ya kutupeleka katika confederation tukiwa mabingwa wa ukanda wetu tunadhani tutafikia malengo msimu huu

www.shaffihdauda.co.tz; Kama kaimu nahodha, unazungumziaje mchezo ujao dhidi ya Yanga SC katika Ngao ya Jamii?

HIMID; Ni mechi ambayo ni muhimu sana na itayobeba hisia nyingi pia ukizingatia hatujawahi kushinda mechi ya ngao hata mara moja, ila naamini kutokana na mbinu za mwalimu wetu, support kutoka kwa uongozi wetu pamoja na utayari wa wachezaji wote naipa nafasi kubwa timu yangu

www.shaffihdauda.co.tz; Kwanini gemu yenu na Yanga katika siku za karibuni zimekuwa na upinzani wa hali ya juu?

HIMID; Nafikiri Azam na Yanga ndiyo timu bora zaidi kwa sasa na pia ndiyo zenye ushindani mkubwa katika kugombea mataji yaliyo ndani ya uwezo wao.

www.shaffihdauda.co.tz; Umekuwa Azam FC tangu ungali kijana mdogo. Misimu 7 VPL, Je, umewahi kufikiriakuondoka hapo?. Au utafuata njia za nyota wa kimataifa walioamua kutengeneza maisha yao katika klabu moja tu.

HIMID; Ningependa kuwa hapa kwa maisha yangu yote ya soka kama sito pata nafasi ya kucheza nje ya nchi, nimekua nikifurahia maisha yangu ya mpira siku zote, japo siwezi jua kitacho tokea mbele ila naamini Mungu ataniongoza katika kutimiza ndoto zangu.

www.shaffihdauda.co.tz; Kila nafasi katika timu imeonekana kuwa na wachezaji wawili hadi watatu,na inapokea; mfano wewe hauko katika mchezo husika, mchezaji mwingine anayepata nafasi hucheza vizuri zaidi. Nini siri ya kila mchezaji wa Azam FC kuwa fit na tayari mudawowote kubeba majukumu ya mwalimu?.

HIMID; Ni kila mtu kujua wajibu wake

www.shaffihdauda.co.tz; Umefanya kazi na walimu tofauti tofauti hapo, unamzungumziaje Stewart Hall?

HIMID; Stew ni mwalimu mzur sana na wa kipekee njia zake ni tofaut sana na walimu wengine, Stew atabaki kuwa Stewart.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.