Saturday, August 8, 2015

KIBOKO YA MABEKI KUREJEA KCCA KWA MKOPO

Posted By: kj - 2:24 PM

Share

& Comment

Kiboko ya mabeki wa upande wa kulia Brian Majwega yuko mbioni kurejea kwa mkopo katika timu yake ya awali ya KCCA ya nchini Uganda inayoshiriki ligi kuu ya Uganda inayo dhaminiwa na Azam TV.

Majwega alihusika katika asilimia kubwa ya mgoli ya Azam FC katika duru la pili la ligi kuu ya vodacom msimu uliopita, ambapo alisajiliwa katika dirisha dogo la usajili akitokea KCCA ya Uganda wakati AZam FC walipoweka kambi ya wiki moja nchini Uganda na wenyeji wao walikuwa KCCA.

Kwa mujibu wa mtendaji mkuu wa KCCA David Tamale, Majwega anatarajiwa kujiunga na KCCA kwa mkopo kabla ya kumalzika kwa wiki hii akitokea Azam FC ambapo kunaonekana kupoteza nafasi.

Tamale aliimbaia mtandao wa Kawowo Sports kuwa wako mbioni kumrejesha kiungo huyu, mahiri kwa upigaji wa krosi na mzuri katika ukabaji katika timu yake aliyotokea kabla ya kujiunga na Azam FC.

"Ni kweli", alisema Tamale alipoulizwa kuhusu kumrejesha Majwega klabuni na kuongeza kuwa "Tupo kwenye makubaliano ya mwisho na matumaini yetu itakuwa sawa kabla ya kuanza wikii ijayo".

Majwega alisajiliwa Azam FC kufuatia kwa kutokuwa fiti mawinga wa kushoto wa Azam FC Farid Mussa, Joseph Kimwaga na Khamis Mcha Viali, kuliko sababishwa na majeraha kuwaandama.

Kuongezwa kwa Ramadhani Singano, urejeo wa Farid Mussa umetishia uwepo wa nafasi ya Majwega katika kikosi cha Azam FC, ambapo hakujumuishwa katika michuano ya kombe la kagame lililomalizika kwa Azam FC kuibuka mabingwa.

Kuondoka kwa Majwega kunatengeneza nafasi kwa Azam FC kusajili mchezaji mwingine wa kimataifa katika dirisha hili la usajili kabla halijafungwa.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.