Saturday, March 10, 2018

YAKUBU NNJE WIKI SITA

Posted By: dada - 12:06 AM

Share

& Comment

BEKI kisiki wa kati wa Azam FC, Yakubu Mohammed, anatarajia kukaa nje ya dimba kwa muda wa wiki sita kuanzia sasa baada ya kufungwa plasta gumu ‘P.O.P’ kwenye mguu wake wa kulia.

Yakubu amefungwa P.O.P baada ya kuvunjika mfupa wa nyuma kwenye kifundo cha mguu katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya KMC ambao Azam FC ilishinda mabao 3-1 na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa, ameuambia mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuwa beki huyo atakaa na plasta hilo gumu kwa muda wa wiki nne kabla ya kwenda kutolewa.

“Kwa muda wa wiki nne atakuwa na P.O.P na baada ya hapo atakapotolewa P.O.P ataanza programu ya kurejesha mwili kwenye hali ya kawaida (rehabilitation) kwa muda wa wiki mbili kwa hiyo kuanzia sasa kwa muda wa wiki sita hatutakuwa na Yakubu Mohammed,” alisema.

Akizungumzia majeraha aliyopata jana mshambuliaji wa Azam FC, Mbaraka Yusuph, wakati timu hiyo ikiichapa Mwadui bao 1-0, daktari huyo bingwa wa tiba za michezo alisema wamempumzisha mchezaji huyo kabla ya kumuangalia hali yake kesho.

“Mbaraka Yusuph jana alipata matatizo ya kugongwa katika msuli wa paja na ni maumivu na leo tumeendelea kumuangalia na kumpumzisha lakini kesho (Jumamosi) tutajaribisha tena kumuangalia yupo katika hatua gani ya maumivu na kuanza mazoezi mepesi mepesi,” alisema.

Yusuph alishindwa kuendelea na mchezo huo dakika ya 24 tu baada ya majeraha hayo na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji Shaaban Idd.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.