Hata hivyo kipa huyo ameibuka na kudai kuwa hakutaka kabisa mikwaju hiyo ambayo iliiponza timu yake ilishindwa kwa mara nne mfululizo kunyakua Ngao ya Hisani kwa kulala mikwaju 8-7 mbele ya Yanga.
Manula amekanusha kutaka timu hizo ziende katika mikwaju ya penalti na kusema alilazimika kufanya hivyo ili kupoozesha mchezo baada ya kuona timu yao inashambuliwa zaidi.
Kipa huyo wa Taifa Stars alidai kuwa, kama kipa ni lazima afahamu kusoma mchezo na kuisaidia timu yako kurejea mchezoni na ndicho alichokuwa anakifanya katika mchezo huo wa juzi.
“Timu yetu ilishambuliwa sana kipindi cha pili, kama kipa nilihitaji kufanya kitu, nilijaribu kupoteza muda kidogo ili kupoozesha mchezo na wachezaji wetu wajipange.
“Tumepoteza kwa mikwaju ya penalti, si jambo baya sana, tumecheza vizuri na tumeendelea kuwa na rekodi ya kutofungwa ndani ya dakika 90, kikubwa ni kujipanga zaidi kwa ajili ya ligi,” alisema Manula.
Chanzo: mwanaspoti
0 Maoni:
Post a Comment