Mfumo huo umeanza kutumika tangu kocha huyo arejee tena kwenye kikosi hicho akichukua nafasi ya Joseh Omog wa Cameroon, kwenye msimu uliomalizika
Akizungumza na Kandanda, jana jijini Dar es Salaam, Hall alisema, mfumo huo ni mzuri kwake kutokana na wachezaji kucheza vizuri.
Alisema kama wachezaji wanaweza kufanya vile anavyotaka yeye hakuna haja ya kukaa chini na kutengeneza mfumo mwingine ambao wanaweza kuutumia.
“Sioni shida kuutumia mfumo huu hata kwenye michezo ya ligi inayokwenda kuanza hivi karibuni. Huu ni mfumo ambao wachezaji wangu wanaucheza kwa uelewano mkubwa ndio maana sioni sababu ya kuubadirisha.
“Ninachokwenda kukifanya hivi sasa ni kuuboresha na kuweka baadhi ya vitu kadhaa ndani ya mfumo huu, lakini sipo tayari kuubadirisha na kuanza kufundisha mfumo mwingine ambao itachukua muda wachezaji kuuelewa na kufanya vizuri kwenye michezo yetu” alisema Hall.
Chanzo: Kandanda.co.tz
0 Maoni:
Post a Comment