Kipre Herman Tcheche akichuana na Juma Said Nyoso |
Katika mchezo wa leo ambao azam fc waliuwanza kwa kusaka goli la mapema na kulisakama lililvyo lango la Mbeya city.
Alikuwa Mudathir Yahya Abas aliyeiandikia Azam FC goli la kwanza katika dakika ya 10, kufuatia uzembe wa mabeki wa Mbeya city ambapo badala ya kuondoa hatari walijikuta wakimtengea Mudathir na kuipa uongozi Azam FC.
Kuingia kwa goli hilo kuliwatuliza Azam FC na kutawal;a vilivyo eneo la kati ya uwanja na kuwafanya Mbeya city kushindwa kufika langoni mwa Azam FC.
Ikiwa zimesalia dakika 10 kwenda mapumziko Mbeya city waliocharuka na kujaribu kutengeneza nafasi kadhaa za kujipatia goli ambapo ziliwezwa kuzimwa na safu ya ulinzi ya Azam FC.
Katika kipindi cha pili Azam FC walirejea kwa kasi waliyoanza nao kipindi cha pili huku mbeya city wakijaribu kusaka kasi waliyoanza maliza nayo kipndi cha kwanza.
Katika dakika ya 52 Kipre Herman Tcheche akitumia vyema pasi ya Salum Abubakari na kuiandikia Azam FC goli la pili.
Kuingia kwa goli hilo kuliwaongezea kasi Mbeya city ya kusaka goli ambapo katika dakika ya 56 Raphael Alfa aliiandikia Mbeya city goli lao la kwanza baada ya kugongeana vyema na Mazanda.
Faridi Mussa Maliki alipoteza nafasi ya wazi ya kuiandika Azam FC goli la 3 akiwa teyari ashampiga chenga kipa wa Mbeya city lakini shuiti lake liliokolewa na beki aliyekuwa amewahi langoni mwao.
Katika dakika 20 za Mwisho Mbeya city walitawala mchezo na kusaka goli la kusawazisha bila mafanikio na kupelkea mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
0 Maoni:
Post a Comment