Saturday, September 26, 2015

AZAM KUSAKA USHINDI WA KWANZA KWA MBEYA CITY NDANI YA CHAMANZI KESHO

Posted By: Unknown - 9:39 PM

Share

& Comment

Uwanja wa utakao tumka kesho katika mchezo kati ya Azam <fc na Mbeya City
Mabingwa wa klabu bingwa Afrika Mashariki na kati Azam FC kesho watakuwa na kibaru cha kutafuta ushindi wa kwanza mbele ya Mbeya city katika uwanja wa Azam complex.

Hii inakuwa mara ya tatu kwa Azam FC na Mbeya city kukutana katika ligi kuu ya vodacom katika uwanja wa Azam complex ambapo katika michezo miwili ya mwisho ilimalizika kwa sare ya magoli.

Kwa mara ya kwanza Azam FC waliwakabili Mbeya city katika uwanja wa Azam Complex ambapo kwa mara ya kwanza uwanja huo ulijaa, ulichezwa novemba 7 mwaka 2013 ambapo mchezo ulimalizika kwa sare ya goli 3-3.

Mchezo wa pili ulichezwa aprili 8 walikutana katika uwanja huo na mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1, wakati mara mbili walizokutana katika uwanja wa Sokoine wa Mbeya Azam FC imeibuka na ushindi katika michezo yote hiyo.

Je kesho Azam FC watapata ushindi wa wa kwanza dhidi ya Mbeya city katika uwanja huo uliopambwa na matangazo ya bidhaa bora za Bakharesa, tukutane Chamanzi Kesho, ama kwenye Azam Sport HD na Azam Two.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.