Saturday, September 12, 2015

AZAM FC WAICHAPA TANZANIA PRISONS, MCHEZO WA UFUNGUZI VPL

Posted By: kj - 6:54 PM

Share

& Comment

Farid Musaa Maliki mfungaji wa goli la pili la Azam FC hii leo
Mabingwa wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC leo wameanza vyema ligi kuu ya vodacom, baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 mbele ya Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam complex.

Katika mchezo huo Azam Fc wakicheza soka la uhakika waliandika goli la kwanza katik dakika ya 39 kupitia kwa Kipre Tcheche na kuipeleka Azam Fc mapuj,ziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha Kwanza Azam FC walipoteza nafasi kadhaa za kufunga goli kupitia kwa Allan Wanga ambapo alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na uzi wa Azam FC hii leo.

Kipindi cha pili kilirejea taratibu huku Azam Fc wakitawala ene la kati ya uwnaja na mchezo kwa ujumla kbla ya Tanzania Prisons kupata goli katika dkaika ya 60 kupitia kwa Jeremia Mussa.

Kuingia kwa goli hilo kuliplekea kocha Stewart Hall kumuita benchi Himid Mudathir Yahya na nafasi yake kuchukuliwa na Himid Mao Mkami, kisha akamtoa Allan Wanga na nafasi yake ikachukuliwa na Amme Ally kabla ya kuingia kwa Ramadhan Singano kuchukuwa nafasi ya Migi.

Dakika ya 81 kiungo chipukizi Farid Mussa Malik alitumia vyema pasi murua ya Salum Abubakari na kuiandika Azam FC goli la pili na kuipatia Azam FC ushindi wa goli 2-1.

Azam FC leo: Aishi Manula, Aggrey Morice, Pascal Wawa, Daivd Mwantika, Erasto Nyoni, Jean Baptista Mugereneza/Ramadhan Singano, Salum Abubakari, Mudathir Yahya/Himid Mao, Allan Wanga/Ame Ally, Kipre Tcheche na Farid Mussa Malik a

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.