Tuesday, September 1, 2015

JKT RUVU WAICHAPA GOLI 2-1 AZAM FC

Posted By: kj - 10:19 PM

Share

& Comment

JKT Ruvu wakishangilia moja ya magoli waliyofunga msimu uliopita Azam complex
Baada ya sare mbili mabingwa wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC leo wamepokea kichapo cha goli 2-1 toka kwa JKT Ruvu mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam complex, ukiwa mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo wa kirafiki JKT Ruvu walikuwa wam mwanzo kupata goli katika dakika ya 8 kupitia kwa Gaudence Mwaikimba, akimalizia mpira uliomshinda kipa Mwadini Ally kufuatia shuti la Ally Amour Janja.

Kuingia kwa goli hilo kuliipa utulivu Azam FC na katika dakika ya 13 Kipre Hermana Tcheche aliisawazishia Azam FC na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Katika kipindi cha pili Azam FC waliongeza kasi ya ushambuliaji huku Khamis Mcha Viali akicheza kwa uwelewano na Kipre Tcheche na kutengeneza nafasi ambazo walishindwa kuzitumia.

Katika harakati ya kujibu mapigo JKT Ruvu walitengeneza nafasi nzuri ya kufunga kupitia kwa Amour Janja ambaye shuti lake la kwanza lilitemwa na Mwadini Ally na mpira kumkuta na kupiga shuti ambalo halikuwa na madhara yoyoyte ile.

Katika dakika ya 84 kukosekana mawasiliano kati ya kiungo Bryson Raphael na Mwadin Ally kuliwazawadia goli la pili kwa JKT Ruvu kupitia kwa Naji Magulu aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Amour Janja na kupelekea mchezo kumalizika kwa JKT Ruvu kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

JKT Ruvu inakuwa timu ya pili kuifunga Azam FC baada ya yanga kupata ushindi katika mchezo wa ngao ya jamii kwa mikwaju ya penati, kitu kinachopelekea kuwa timu ya kwanza kuifunga Azam FC toka Hall arejee ndani ya dakika 90.

Kikosi cha Azam FC: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Aggrey Morice, Pascal Wawa, Diouf/Said Morad 46',Gaerdiel Michael, Bryson Raphael, Salum Abubakari, Ramadhan Singano/Khamis Mcha 60', Kipre Tcheche, Amme Ally/Shabaan Idd 65'

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.