Saturday, August 29, 2015

AZAM WATOA SARE NA NDANDA FC, MWANTIKA AKIZAWADIWA KADI NYEKUNDU

Posted By: kj - 7:24 PM

Share

& Comment

David Mwantika akiwa kazini katika moja ya mechi dhidi ya Simba SC, leo alitolewa kwa kadi nyekundu
Mabingwa wa klabu bingwa Afrika masharik na kati Azam FC leo wametoka sare ya goli 1-1 na Ndanda FC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Nagnwanda sijaon mkoani Mtwara.

Katika mchezo huo wa leo Azam FC walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Kelvin Friday katika dakika ya 12 na kuipeleka Azam FC mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Katika dakika ya 70 David Mwantika alizawadiwa kadi nyekundu na Ndanda FC kupatiwa penati ambayo Kigi Makasi aliipaisha.

Katika dakika ya 80 Ndanda FC walifanikiwa kupata goli lao la kusawazisha kupitia kwa Omar Mponda na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Kikosi cha Azam FC kilichopo Mtwara kinatarajiwa kurejea Dar es salaam kesho na siku ya jumanne kucheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja wa Azam complex. 

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.