NAHODHA wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ amesema wataifunga Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE, Bocco amesema kwamba wanaijua vizuri Yanga SC na wataifunga Jumamosi.
“Tunawajua Yanga, ni timu nzuri kweli. Lakini sisi tunajua namna ya kuwafunga. Na tutawafunga tu,”amesema.
Bocco amesema kwamba makosa waliyofanya katika mechi mbili zilizopita walizokutana na Yanga SC kumaliza dakika 90 bila kufunga bao, hawawezi kuyarudia.
Mechi mbili za awali msimu huu kuzikutanisha Yanga na Azam FC kila timu ilishinda moja, tena kwa mikwaju ya penalti.
Azam FC ilianza kuifunga Yanga SC kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame Julai mjini Dar es Salaam.
Na Yanga SC ikalipa kisasi kwa ushindi wa penalti 8-7 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika mchezo wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Taifa Agosti mwaka huu.
Jumamosi zikikutana kwa mara ya tatu, utakuwa mchezo wa kuwania usukani wa Ligi Kuu na pia kumaliza ubishi wa nani zaidi baina yao.
Kwa ujumla Ligi Kuu inandelea Jumakosi kwa mechi sita kupigwa kwenye viwanja tofauti na mbali na Yanga SC kumenyana na Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Chanzo: Habari leo
0 Maoni:
Post a Comment