Friday, January 1, 2016

AGGREY KWENDA SAUZI SIKU YA MAPINDUZI, NNJE MIEZI 3

Posted By: kj - 10:54 AM

Share

& Comment


Beki tegemeo wa Azam, Aggrey Morris ameuanza mwaka huu vibaya baada ya kutakiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu akiuguza majeraha ya goti ambapo uongozi wa timu hiyo umepanga kumpeleka Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi.

Aggrey alikumbana na majeraha hayo alipokuwa akikichezea kikosi cha taifa cha Zanzibar, Zanzibar Heroes, katika michuano ya Kombe la Chalenji, Novemba, mwaka jana nchini Ethiopia.

Msemaji wa timu hiyo, Jaffar Idd 'Mbunifu', kuwa beki huyo atapumzika kwa kipindi hicho kutokana na kutaka kumpa matibabu kamili kabla ya kurejea tena uwanjani kuungana na wachezaji wenzake.

“Tutamkosa Aggrey kwa miezi mitatu lakini ndani ya kipindi hicho, uongozi utampeleka Afrika Kusini kupata matibabu ambayo yatamrejesha kwenye hali yake ya kawaida, safari yake inatazamiwa kuwa Januari 12, mwaka huu,” alisema Maganga.

Awali, Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall aliiambia SALEHJEMBE kwamba aliamua Morris afanyiwe vipimo vyote ili kupata uhakika wa kinachomsumbua ili kipatiwe ufumbuzi.

"Maana imekuwa kila baada ya matibabu, siku chache anaumia tena. Sasa nimeagiza uchunguzi wa kina ili kujua tatizo na mwisho lipatiwe ufumbuzi," alisema Hall.

cHANZO: SALEH JEMBE BLOG

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.