Akizungumza na mtandao wa www.azamfc.co.tz Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, alisema kuwa kikosi hicho kitaondoka nchini kesho usiku kwa usafiri wa ndege mara baada ya kumaliza mchezo wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya African Lyon.
“Tutatumia michuano hiyo kama maandalizi yetu ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na tunaamini itatusaidia vilivyo kukabiliana na mashindano yaliyopo mbele yetu,” alisema
Kawemba aliwatoa hofu mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa wakiifuatilia timu hiyo popote inapokuwa kwenye mechi zake nchini kwa kuwaambia kuwa watapata kushuhudia burudani ya mechi za Azam FC katika mechi zao huko kupitia televisheni ya Azam TV.
Azam FC itaanza kuwania taji la michuano hiyo kwa kucheza na Zesco United Jumatano ijayo saa 10.00 jioni kwa saa za hapa, huku mchezo wa ufunguzi utakaoanza saa 8.00 mchana ukiwahusisha Zanaco watakaokipiga na Chicken Inn.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati watateremka tena dimbani saa 8.00 mchana Jumamosi ijayo kwa kukipiga na mabingwa wa Zimbabwe Chicken Inn, huku ukifuatiwa na ule baina ya wapinzani wa nchini humo Zesco na Zanaco utakaopigwa saa 10.00 jioni.
Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB, itamalizia mechi yake ya mwisho Februari 3 mwaka huu kwa kukipiga na Zanaco, mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni, utakaotanguliwa na ule baina ya Zesco na Chicken Inn utakaoanza saa 8.00 mchana.
0 Maoni:
Post a Comment