Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC wameanza kwa sare michuano ya kombe la mapinduzi, baada ya kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Mtibwa sugar mchezo uliochezwa katika uwanja wa Amani visiwani Zanzibar.
Azam Fc wakianza na kikosi ambacho akijazoeleka kuanza kwa wachezaji wengi waliokuwa wanasugu benchi ama kuka jukwaani katika michezo iliyopita ya ligi kuu ya vodacom na ile ya klabu bingwa afrika mashariki wakipewa nafasi hii leo.
Azam F waliwanza vyema mchezo kabla ya Mtibwa sugar kuweka mchezo katika himaya yao katika dakika ya 5 mpaka dakika ya 25 ya mchezo, ambapo Azam FC walirejea mchezoni taratibu.
Azam FC katika kipindi cha kwanza walifanya majaribio mawili langoni mwa mtibwa sugar na kufanikiwa kupiga kona mbili wakati mtibwa sugar wakifanya majaribio manne ambayo yote yalitokaa nnje ya goli.
Burudani katika kipindi cha kwanza ilikuwa baina ya viungo waliokwisha wahi kucheza pamoja Mudathir Yahya na Ibrahim Jeba ambapo kila mmoja katika nyakati tofsuti aliichezesha vyema timu yake.
Ushindani huo wa Jeba na Muda ulikwisha kipindi cha pili baada ya Stewart Hall kuamua kumingiza Franky Domayo kuchukuwa nafasi ya Khamisi Mcha kitendo kilichopelekea kusogea kwa mbele Mudathir Yahya.
Katika dakika ya 61 Mtibwa sugar waliandika goli la kuongoza likifungwa na Husein Javu akimalizia pasi safi ya Ramadha Kichuya aliyetumia vyema makosa ya David Mwantika.
Nahodha John Bocco akitokea benchi, katika dakika ya 73 aliangusha katika eneo la hatari na kupelekea kupigwa kwa penati ambayo Bocco alikwamisha nyavuni na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Katika mchezo wa leo umemshuhudia beki Waziri Salum akirejea uwanjani kwa mara ya kwanza baaada ya kuka nje ya uwanja kwa takribani miaka miwili, akiuguza jeraha lake, na leo akicheza mchezo wake wa kwanza wa mashindano toka mwaka 2013.
Azam FC leo: Mwadini Ally, Abdallah Kheri, Said Moradi, David Mwatika, Gardiel Michael/Waziri Salum, Himidi Mao/Jean Mugereneza, Khamisi Mcha/Franky Domayo, Mudathir Yahya, Ame Ally/Kipre Tcheche, Allan Wanga/John Bocco na Ramdhan Singano.
0 Maoni:
Post a Comment