Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC leo wamefanikiwa kupata ushindi dhidi ya mabingwa wa Zimbabwe Chiken Inn katika mchezo wa kirafiki uliochezwa mjini Ndola Zambia.
Katika mchezo huo Chiken Inn walikuwa wa mwanzo kuandika goli kabla ya nahodha wa Azam FC John Raphael Bocco kuisawazishia Azam FC katika dakika ya 34 na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.
Azam FC waliandika goli la pili kupitia kwa Kipre Herman Tcheche kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 54, kabla ya Chiken Inn kujifunga katika dakika ya 64 na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 3-1..
Azam FC watahitimsha ziara yao siku ya jumatano kwa kucheza mchezo mmoja dhidi ya wawakilishi wa Zambia katika kombe la shirikisho Zanaco FC.
0 Maoni:
Post a Comment