MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu, anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, leo amenusurika katika ajali mbaya, lakini gari yake aina ya Toyota Premio ‘halitamaniki’.
Kavumbangu ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba ajali hiyo imetokea leo asubuhi wakati anatoka nyumbani kwake, Kijichi kwenda hospitali ya Dk Gilbert, Mikocheni kwa matibabu ya majeruhi yake yanayomuweka nje tangu mwezi uliopita.
Amesema wakati anakata kona kwenye mzunguko wa magari yanayotoka Kijichi na Mbagala kuelekea mjini, ndipo alipogongwa na gari kubwa la mizigo, ambalo ‘limeiharibu sura’ gari yake kwa mbele.
“Kisheria inatakiwa wale wanaotoka Mbagala watusubiri sisi tunaozunguka tupite, lakini jamaa hakusimama akapita na moto akaipitia gari yangu kwa mbele yote imeharibika sura,”amesema.
Na Kavumbangu anasikitika jamaa baada ya kugonga hakusimama akakimbia na hakukuwa na trafiki karibu wa kuja japo kupima ajali.
“Kwa kuwa mimi sikuumia, nikaona hapa nitapoteza muda bure, nikaita gari la kuvuta gari yangu, mimi nikaenda zangu kwa Dokta Gilbert,”amesema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC.
Chanzo: BIN Zubeiri
Kavumbangu ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba ajali hiyo imetokea leo asubuhi wakati anatoka nyumbani kwake, Kijichi kwenda hospitali ya Dk Gilbert, Mikocheni kwa matibabu ya majeruhi yake yanayomuweka nje tangu mwezi uliopita.
Gari ya Didier Kabumbangu (picha ndogo kulia) inavyoonekana kwa mbele baada ya ajali |
Mipira ya kumzuia aliye ndani ya gari asiumie ikiwa imechomoka kutokana na ajali hiyo |
Amesema wakati anakata kona kwenye mzunguko wa magari yanayotoka Kijichi na Mbagala kuelekea mjini, ndipo alipogongwa na gari kubwa la mizigo, ambalo ‘limeiharibu sura’ gari yake kwa mbele.
“Kisheria inatakiwa wale wanaotoka Mbagala watusubiri sisi tunaozunguka tupite, lakini jamaa hakusimama akapita na moto akaipitia gari yangu kwa mbele yote imeharibika sura,”amesema.
Didier Kavumbangu amekuwa nje tangu mwezi uliopita kutokana na majeruhi |
“Kwa kuwa mimi sikuumia, nikaona hapa nitapoteza muda bure, nikaita gari la kuvuta gari yangu, mimi nikaenda zangu kwa Dokta Gilbert,”amesema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC.
Toyota Premio ya Kavumbangu inavyoonekana kikamilifu baada ya ajali leo |
0 Maoni:
Post a Comment