Wednesday, January 27, 2016

KOCHA WA MAKIPA TOKA KENYA: MANULA NDIYE BORA KWA SASA TANZANIA

Posted By: kj - 10:53 AM

Share

& Comment


Kipa wa Azam FC, Aishi Manula, ametajwa kuwa ndiye kipa bora katika Ligi Kuu Bara msimu huu mpaka sasa akiwapiku makipa kadhaa akiwemo, Deogratius Munishi ‘Dida’ wa Yanga na Juma Kaseja wa Mbeya City.

Kwa mujibu wa aliyekuwa kocha wa zamani wa makipa wa Simba, Mkenya, Iddi Salim, kwa kipindi cha miezi sita alichokaa Tanzania kufundisha soka, amemuona Manula kuwa ndiye bora huku akisisitiza kama ataendelea kulelewa kwenye misingi bora, bila shaka atakuja kuwa msaada mkubwa kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

 “Kwa miezi sita niliyokaa Tanzania, naweza kusema nimewaona makipa wengi katika Ligi Kuu Bara, lakini kipa wa Azam, Manula, kwangu ndiye ni bora zaidi kuliko mwingine kutokana na mambo anayoyafanya uwanjani ikiwemo kucheza penalti nyingi.

“Lakini pia ukiangalia kwa makipa vijana, Manula anashika namba moja akifuatiwa na Manyika, na kama watazidi kukomaa basi watakuja kuwa makipa wazuri siku za usoni,” alisema kocha huyo aliyewahi kuinoa Gor Mahia na timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars'.

Akizungumzia kipa mwingine bora, Idd alisema Peter Manyika wa Simba, kama atapata matunzo mazuri, mafunzo mazuri na kuthaminiwa, ndiye atakuwa tegemeo la Tanzania hapo baadaye.

Chanzo: salehjembe blog

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.