Monday, February 8, 2016

AGGREY, KAVUMBAGU KUANZA MAZOEZI KESHO

Posted By: kj - 8:45 PM

Share

& Comment


WACHEZAJI wawili wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, beki Aggrey Morris na mshambuliaji Didier Kavumbagu, wanatarajia kuanza mazoezi rasmi kesho baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakiwakabili.

Morris alikuwa akisumbuliwa na mejeraha ya goti tokea Novemba mwaka jana alipoumia alipokuwa kwenye kikosi cha timu yake ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes', iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji.

Mwezi uliopita alipelekwa jijini Cape Town nchini Afrika Kusini katika Hospitali ya Afrisurb kufanyiwa matibabu na kutakiwa kupumzika kwa takribani wiki tatu kabla ya kuanza mazoezi.

Kwa upande wake Kavumbagu alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya enka aliyopata wakati wa mchezo wa Kombe la Mapunduzi mwezi uliopita dhidi ya Yanga, ulioisha kwa sare ya bao 1-1.

Akizungumza na mtandao wa www.azamfc.co.tz  Daktari wa Azam FC, Juma Mwimbe, alisema Morris ataanza na mazoezi ya gym kesho kwa muda wa wiki moja kabla ya kuhamia kwenye mazoezi mepesi ya uwanjani kwa muda wiki moja pia.

"Yote hayo ni ya kumweka fiti kwa kuwa alikosa mechi muda mrefu. Baada ya hapo ataanza mazoezi na wenzake uwanjani mara baada ya sisi kurejea kutoka mechi za Mbeya (Mbeya City na Tanzania Prisons," alisema.

Mwimbe alisema Kavumbagu naye ataanza na mazoezi ya gym kesho, ambayo atafanya kwa siku kadhaa kabla ya kuanza mazoezi na wenzake uwanjani.

"Kavumbagu programu yake ya kurejea uwanjani ni fupi kwa kuwa hajakaa nje muda mrefu," alimalizia Mwimbe.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.