KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, itakuwa nje ya uwanja wake wa nyumbani ‘Azam Complex’ kwa takribani mwezi mmoja.
Azam FC itatumia muda wote huo kucheza mechi ugenini, ambapo mchezo wa mwisho kutumia uwanja wa nyumbani ni ule walioichapa Mwadui ya Shinyanga bao 1-0 Februari 7, 2016.
Mabingwa hao wa Kombe la Kagame, watatumia muda wote huo ugenini kucheza mechi tano, kati ya hizo nne ni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na mmoja ukiwa wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya Panone FC ya mkoani Kilimanjaro.
Azam FC itaanza kucheza mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Coastal Union ya Tanga Jumapili ijayo (Februari 14) katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga kabla ya kuelekea jijini Mbeya kucheza na Mbeya City (Februari 20) na Tanzania Prisons (Februari 24).
Baada ya kumaliza kibarua chake hicho, itaelekea moja kwa moja jijini Moshi, Kilimanjaro kumenyana na Panone katika mchezo wa raundi ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) utakaofanyika Uwanja wa Ushirika Februari 28, 2016.
Kama hiyo haitoshi itarejea jijini Dar es Salaam na siku sita baadaye (Machi 5, 2016) itashuka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuvaana na wenyeji wao, Yanga.
Azam FC yaelekea Tanga
Wakati huo huo, kikosi cha timu ya Azam FC kinatarajia kuondoka leo mara baada ya mazoezi ya asubuhi kuelekea mkoani Tanga kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Coastal UnionRATIBA YA AZAM FC UGENINI:
Coastal Union vs Azam FC (Februari 14, 2016 Uwanja wa Mkwakwani)Mbeya City vs Azam FC (Februari 20, 2016, Uwanja wa Sokoine)
Tanzania Prisons vs Azam FC (Februari 24, 2016, Uwanja wa Sokoine)
Panone FC vs Azam FC (Februari 28, 2016 Uwanja wa Ushirika)
Yanga SC vs Azam FC (Machi 5, 2016, Uwanja wa Taifa)
0 Maoni:
Post a Comment