Thursday, March 31, 2016

AZAM ACADEMY WAFUNGWA FOLI 3-2 NA TIMU YA TAIFA U17

Posted By: dada - 3:35 PM

Share

& Comment

KIKOSI cha vijana cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC ‘Azam Academy’ kimepoteza mchezo kwa mara ya kwanza tokea kuanza mwaka huu, baada ya kufungwa mabao 3-2 na timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Karume leo saa 2.00 asubuhi.

Mchezo huo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya Azam kuisapoti timu hiyo ya Taifa inayonolewa na kocha kutoka Denmark, Kim Poulsen, ambayo inajiandaa na mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Misri, wa kwanza ukifanyika keshokutwa Jumamosi na mwingine Jumanne ijayo.

Serengeti Boys ndio walikuwa wa kwanza kupata mabao mawili katika kipindi cha kwanza, yaliyofungwa na Ali Msengi, Maziku Aman na kufanya mpira huo kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa mabao hayo.

Kipindi cha pili Azam Academy ilirejea mchezoni na kuanza kulisakama lango la Serengeti Boys na kufanikiwa kupata bao la kwanza, lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na beki Abbas Kapombe kufuatia mshambuliaji Shabaan Idd kuangushwa ndani ya eneo la 18.

Azam Academy iliendelea kuliandama lango la wapinzani wao, hali iliyowafanya kuandika bao la kusawazisha lililofungwa na Yahaya Zaid aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Yohana Mkomola.

Uzembe wa dakika za mwisho uliofanywa na mabeki wa Azam Academy uliigharimu baada ya Serengeti Boys kuandika bao la tatu lililotiwa wavuni na Rashid Chambo kwa shuti kali ndani ya eneo la 18 baada ya kumzidi maarifa beki Abbas Kapombe.

Hivyo hadi dakika 90 zinamalizika Serengeti Boys iliweza kutoka kifua mbele kwa ushindi huo.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.