Sunday, April 17, 2016

KIKOSI CHA MAANGAMIZI CHATUA SALAMA TUNISIA

Posted By: Unknown - 5:21 PM

Share

& Comment

KIKOSI cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, kimewasili salama jijini Tunis, Tunisia leo saa 7.30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki kwa ajili ya kupambana na wenyeji wao Esperance.

Mchezo huo wa marudiano wa raundi Kombe la Shirikisho Afrika utafanyika kwenye Uwanja wa Uwanja wa Olympique de Rades keshokutwa Jumanne Aprili 19 saa 3.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (saa 1.00 usiku kwa Tunisia).

Azam FC iliyosafiri kwa takribani saa 11 kutoka Dar es Salaam jana saa 10.45 jioni hadi Dubai ilipopumzika kwa takribani saa tatu kabla ya leo asubuhi kuanza safari ya kuelekea Tunisia ilipowasili saa 7.30 mchana na kupokelewa viongozi wa timu hiyo, Mwenyekiti Said Mohamed, Makamu Mwenyekiti Idrissa Nassor na Ofisa Mtendaji Mkuu Saad Kawemba.

Mara baada ya kuwasili kikosi hicho kimefikia kwenye Hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya El Mouradi Gammarth iliyopo La Marsa, jijini Gammarth, Tunisia.


Hakuna kulala

Kwa mujibu wa programu ya Benchi la Ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu Stewart Hall, mara baada ya kuwasili hapa kikosi hicho kitapumzika kwa takribani kwa saa sita kuondoa uchovu na saa 3.00 usiku kwa saa Afrika Mashariki (sawa na saa 1.00 usiku kwa saa za Tunisia) kitafanya mazoezi ya kwanza jijini humo.

Kama sheria za CAF na FIFA zinavyosema, Azam FC kesho itaendelea na programu yake kwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Olympique de Rades utakaotumika kwa mchezo huo.

Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB inahitaji sare yoyote au ushindi ili iweze kusonga mbele kwa hatua ya 16 bora (play off), itakapokutana na moja ya timu iliyotoka kwenye hatua hiyo ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ikifuzu hapo itatinga moja kwa moja katika hatua ya makundi ya michuano hiyo (robo fainali).

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.