Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz hivi karibuni, Jose alisema kuwa jambo kubwa wanalokosa ni mbinu, hivyo amejipanga kulifanyia kazi suala hilo.
“Azam ni timu nzuri na ina uwezo mkubwa sana, kiwango cha makipa niliowakuta kipo vizuri, cha muhimu ni kujituma zaidi na kuzidisha mbinu ili wawe bora zaidi kwa baadaye,” alisema.
Tanzania vs Hispania
Kocha huyo hakusita kuelezea utofauti wa makipa kutoka Tanzania na Hispania mara baada ya kuwaona wa Azam FC, ambapo alisema magolikipa wa hapa wana nguvu sana lakini wanakosa mbinu.
“Watanzania wana nguvu sana, ila wanakosa mbinu, lakini kwa upande wa kule Hispania wako vizuri zaidi na wanazo mbinu, na hicho ambacho nimeongea na wenzangu ili tuweze kukifanyia kazi,” alimalizia kocha huyo mwenye umbile kubwa na mrefu atayesaidiana majukumu hayo na Idd Abubakar.
Ukiondoa makipa wa Azam FC, Aishi Manula, Mwadini Ally na Metacha Mnata aliyepandishwa kutoka timu ya vijana na Kauju Agustino wa Azam B wanaendelea kufanya maandalizi ya msimu mpya, kuna makipa wengine wawili wa kigeni wanawania nafasi moja ya kusajiliwa, Daniel Yeboah (Ivory Coast) na Juan Jesus Gonzalez (Hispania).
Mabingwa hao wanaingia tena sokoni kutafuta golikipa mara baada ya kuachana na kipa mkongwe Ivo Mapunda, aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo msimu uliopita, ambapo anasajiliwa mwingine kuziba nafasi yake ili kuimarisha zaidi kikosi na kuleta ushindani zaidi kwenye nafasi hiyo.
0 Maoni:
Post a Comment