Baada ya Ligi ya Azam ya Vijana chini ya umri wa miaka 15 (Azam Youth League U-15) iliyotarajiwa kuanza leo Jumamosi kuahirishwa kwa wiki moja zaidi hadi Oktoba 14 kutokana na baadhi ya timu shiriki kutothibitisha umri kwa wachezaji wake, timu za vijana za Azam FC U11, 13 na 15 zimetumia siku hii kwa kucheza mechi za kirafiki.
Timu hizo leo zilipata ugeni wa kutembelewa na kituo cha kukuza vipaji cha External Academy FC na kucheza nao mechi mbalimbali za kujiweka sawa baada ya mazoezi ya wiki chini ya Mkuu wa MAendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg.
Vikosi hivyo vya vijana vya Azam FC, vimefanikiwa kuibuka na ushindi katika mechi hizo; Azam U-11 ikiichapa External U-11 mabao 2-1, Azam FC U-13 ikaibugiza External U-13, 2-0, huku External U-15 ikipigwa 3-0 na vijana wa Azam FC U-15 katika mchezo uliokuwa wa kuvutia kutokana na umahiri wa timu hiyo ya vijana ya Azam.

0 Maoni:
Post a Comment