Tuesday, July 12, 2011

Ngassa: aomba dua zenu

Posted By: azam fans - 10:52 AM

Share

& Comment

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anaechezea Azam FC, Mrisho Khalfan Ngassa aliwasili salama nchini Marekani na jana alitazamiwa kuanza majaribio yake na Klabu ya Seatled Soundown.

Mtu aliyeongozana na Mrisho Ngassa aliiambia blog ya Michuzi kuwa Ngassa anaomba dua zenu iliafanye vyema katika majaribio yake ya wiki moja na anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi kitakacho wakabili Manchester United.

Ngassa alipata nafasi katika timu hiyo inayoshika nafasi ya pili katika ligi ikiwa nyuma ya LA Galaxy anayochezea Muingeleza David Beckahm, baada ya kuonekana katika michezo ya kimataifa aliyo shiriki na timu ya Taifa na baadhi ya michezo ya Azam FC.


Wakati huo huo kikosi B cha Azam FC kili ichakaza goli 4 kwa bila timu CIDC siku ya jumapili katika michuano ya vijana inayo andaliwa na kituo cha Rollingstone yanayo endelea mkoani Arusha.

2 Maoni:

  1. inshallah kwa uwezo wa mungu

    ReplyDelete
  2. natafuta yzi wa chama letu huu wa azam cola

    ReplyDelete

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.