MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Mrisho Ngassa ataanza katika kikosi cha kwanza cha timu Seattle Sounders itakapopambana na Manchester United kwenye Uwanja wenye nyasi bandia wa CenturyLink ikiwa ni mchezo wa kirafiki.
Manchester iko Marekani ikijinoa kwa mechi za kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu ya England baadaye mwezi ujao. Mwandishi wa Habari wa Seattle Sounders, Joshua Mayers aliiambia Mwananchi hapa Nairobi kuwa Ngassa ni kati ya wachezaji wanaotarajiwa kuwa katika kikosi cha kwanza katika mchezo wa (leo) utakaoanza saa1:00 saa za Seattle, Marekani sawa na saa 8:00 usiku saa zaTanzania.
"Ninachoweza kukwambia ni kwamba, hakuna kilichobadilika, Ngassa atacheza mechi hiyo...kama mlivyoelezwa basi itakuwa hivyo, siwezi kukupangia kikosi kitakachocheza kwa kuwa kocha hajatangaza, lakini Ngassa yumo kikosini," alisema Mayers kutoka mji wa Seattle, Marekani.
Alisema kuwa Ngassa amekuwa gumzo katika viunga vya Seattle na kila mmoja anataka kumuona katika mchezo huo wa Manchester United ikiwa ni mechi ya kwanza kubwa mwaka huu.
Ngassa aliyekuwa akikipiga katika klabu ya Azam, alikwenda Marekani wiki iliyopita kwa ajili ya majaribio ya wiki mbili na endapo atafuzu, atakuwa mchezaji wa kwanza waTanzania kujiunga na klabu hiyo ya Marekani iliyowahi kufanya ziara Tanzania mwaka 2008.
Juzi Jumatatu, Sounders FC iliyoshinda mechi 11 za ligi na kirafiki bila kupoteza hadi sasa, ilikuwa ikifanya mazoezi kwenye Viwanja vya Microsoft vya Redmond na yalikuwa mazoezi maalum kwa ajili yakuwaonyesha mabosi na viongozi mbalimbali wa timu pamoja na familia zao kuja kuwaona wachezaji wao.
Timu ilikuwa katika mazoezi ya kawaida, iligawanywa katika makundi manne, wakifanya mazoezi ya wanne wanne na baadaye kutengeneza timu kwa mazoezi ya watano watano huku wachezaji wakifunga upande wowote wanao karibia.
Jana Sounders ilifanya mazoezi kwenye uwanja wake wa Starfire tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya Manchester United utakaopigwa CenturyLink. Kocha mkuu wa timu hiyo, Sigi Schmid ambaye aliwashukuru wadhamini mbalimbali kuidhamini timu yake, aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao. "Wachezaji wanapoona umati wa mashabiki, wanapata nguvu zaidi, nadhani itakuwa vizuri wakija kwa wingi.
copied from mwananchi.co.tz
Wednesday, July 20, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment