Thursday, July 21, 2011

Usafiri wapelekea mchezo kuchezwa dakika 30

Posted By: kj - 12:22 PM

Share

& Comment

Japo kuwa mchezo umechezwa dakika 30 Azam FC wameweza kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana, Azam Stadium jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo umedumu kwa nusu saa kutokana na timu ya Ruvu Shooting Stars kuchelewa kufika akitokea Mlandizi mkoa wa Pwani ambako ni makazi ya timu hiyo.

Katika mchezo huo Azam FC walipata goli hilo dakika ya nne ya mchezo ikiwa ni mpira wa adhabu uliopigwa na mchezaji Hamis Mcha. Goli hilo la mapema lilibadili mchezo na kuwa mzuri na wa kasi kwa timu zote kushambuliana huku Ruvu Shooting waki kosa nafasi kwa kupiga mashuti yaliyo kuwa yaki toka nje na mengine kuokolewa na kipa Obrein Cirkovic, wachezaji Michael Norbert na Yusuph Mgwao walishindwa kutumia nafasi hizo.

Upande wa Azam FC, mshambuliaji Wahab Yahya alikosa goli la wazi akiwa yeye na kipa, huku mchezaji Kipre Tcheche alionekana mwiba kutokana na uwezo wake.

Kutokana na kuchezwa kwa muda mfupi, mchezo huo ulio hudhuriwa na mamia wa wapenzi wa Azam FC na kujaza majukwaa yote unatarajiwa kurudiwa siku ya Jumatano ya wiki ijayo.

Azam FC itaondoka Ijumaa kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mechi yake ya tatu ya majaribio dhidi ya Coastal Union, mchezo utakaochezwa uwanja wa Mkwakwani, Azam FC ilicheza mechi yake ya kwanza ya kirafiki na kuibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Villa Squad wiki iliyopita.

Azam FC, Obren, Erasto, Waziri, Nafiu, Aggrey, Mwaipopo, Himid Mao/Salum Abubakar, Jamal Mnyate, Ramadhan Chombo, Khamis Mcha/Wahab Yahya, Kipre Tchetche/Zahoro Pazi.


Copied from azamfc.co.tz

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.