Kikosi cha wachezaji 20 wa AzamFC kiko njiani kikielekea mkoani Arusha kwa ajili ya kucheza mchezo wake wa tatu wa ligi kuu ya Vodacom VPL dhidi ya timu ya JKT Oljoro.
Azam FC ilikuwa wacheze mchezo huo siku ya Jumatano ya wiki hii katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid uliopo Arusha. Lakini taarifa za uhakika toka TFF zinasema kuwa mchezo huo umeseogezwa mbele hadi Ijumaa september 9 na mchezo kati ya Azam na Simba utachezwa september 11 badala ya 10 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema matayarisho kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika kinachosubiliwa ni mechi yenyewe. Amesema kutokana na mechi hio kuchezwa katika uwanja wanyasi za kawaida, timu ilifanya mazoezi ya siku tatu katika kiwanja cha nyasi za kawaida kilichopo Kawe, ili kujiweka sawa na mchezo huo.
“niliwabadilishia uwanja iliwapate mazoezi yatakayo wasaidia kucheza katika viwanja vya kawaida, wameonyesha kumiliki mazoezi hivyo napata uhakika wa kufanya vizuri katika mchezo huo.” Alisema Stewart.
Ameongeza kuwa timu itasafiri na wachezaji 20, kwa kuwa Abdulhalim Humud alipata majeraha, Salum Aboubakar ‘SureBoy’ anatumikia adhabu ya kadi nyekundu na Himid Mao anajiandaa na mitihani ya kumaliza kidato cha nne.
Wachezaji watakao kuwepo katika msafara huo ni Obren Curcovic, Mwadin Ally, Malika Ndeule, Wazir Salum, Ibrahim Shikanda, Ibrahim Mwaipopo, Aggrey Moris, Jabir Aziz, Zahor Pazi, John Bocco, Nafiu Awudu, Wahab Yahya, Mrisho Ngassa, Luckson Kakolaki, Ramadhan Chombo, Said Morad, Kipre Tchetche, Khamis Mcha na Erasto Nyoni.
Katika msafara huo kocha ataongozana na wasaidizi wake, Kali Ongala na Idd Aboubakar. Pia katika safari hiyo yumo Meneja msaidizi Khamis Jaffar, Dr Twalib Mbaraka, na Jaffar Iddi Maganga.
Azam FC wamecheza michezo miwili, wamepoteza mchezo mmoja kwa Africa Lyon na kushinda mchezo dhidi ya Moro United, imefikisha pointi tatu.
www.azamfc.co.tz
Tuesday, September 6, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment