Tuesday, November 8, 2011

Azam kusajili washambuliaji

Posted By: kj - 8:23 PM

Share

& Comment

KOCHA wa Azam FC, Stewart Hall, amesema wamesitisha mikataba ya Waghana, Wahabu Yahya na Nafiu Awudu, kwani wamekuwa wakila bure fedha za klabu hiyo.

Na sasa kocha huyo anasema wanajipanga kusajili washambuliaji watatu katika kipindi cha dirisha dogo la usajili.

Tutafanya hivi kwa kwa safu yetu ya ushambuliaji haina makali kutosha. Kama ujuavyo mshambuliaji kazi yake ni kufunga mabao na si vinginevyo, alisema Hall.

Akizungumzia kwa undani sababu za kuamua kuachana na Waghana hao, Hall alisema haoni sababu ya kuendelea kuwa nao kwani mchango wao kwenye timu ni mdogo, usiolingana na malipo makubwa wanayopewa.

Fedha wanazolipwa wao zinaweza kutumiwa na wachezaji wengine wenye manufaa kwa timu, alisema.

Tunataka kuwa na wachezaji wanaojua wajibu wao na wanoweza kuutimiza wajibu huo.

Kuhusu ni wapi anakusudia kuwapata wana ndinga hao wapya, alisema kuwa mchezaji yeyote mwenye uwezo mkubwa atamsajili awe anatoka ndani au nje ya nchi.



mwanaspot

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.