Tuesday, December 20, 2011

Azam waichabanga goli 2 yanga

Posted By: kj - 7:52 PM

Share

& Comment


Wachezaji wa Azam FC walio wahi kutamba na uzi wa Kagera Sugar pamoja na Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa na Gaudence Mwaikimba ndiyo waliyowapa ushindi Azam FC leo katika uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo maalumu kwa ajili ya kuchangisha pesa za kukomboa viti vya walemavu vilivyokwama bandarini uliwashuhudia Kipre Bolou, Abdi Kasim na Gaudence Mwaikimba wakivaa uzi wa Azam FC kwa mara ya kwanza.

Katika mchezo huo ambao kipa wa Yanga Yarw Berko alifanya kazi yaziada kuokoa mashambulizi ya Azam ulishuhudia mabadiliko ya mapema dakika 39 kwa upande wa Yanga baada ya kutolewa Stephen Mwasika aliyekuwa anarejea toka kwenye majeraha yaliyo muweka nnje mda mrefu na nafasi yake kuchukuliwa na Abuu Ubwa.

Azam FC wakicheza bila ya mshambuliaji tegemeo na tishio John Raphael Bocco 'Adebayor' iliwachukuwa dakika 44 kupata goli la kuongoza lililowekwa kimiani na Gaudence Mwaikimba kwa mkwaju wa penati, baada ya kufanyiwa faulo Mrisho Ngassa katika eneo la hatari.

Azam FC walikwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa goli moja, na kipindi cha pili kilianza kwa kufanywa mabadiliko ambapo alitoka Humud na kuingia Salum Abubakary pamoja, Zahoro Pazi nafasi ya Kipre Tchetche na Jabir Azizi nafasi ya Kipre Bolou.

Wakati yanga walimtoa Pius Kisambale dakika ya 51 na kuingia Hamis Kiiza na dakika 54 Idrisa Rashidi alichukua nafasi ya Athuman Iddi Chuji, dakika mbili kabla ya Mrisho Ngassa kuhitimisha magoli kwa kuifungia Azam goli 2, na dakika ya 75 alimpisha Khamisi Mcha Vuai.

Mpaka kipenga cha Mwisho kina pulizwa Azam 2-0 yanga. Azam mchezo huo ni maandalizi ya kuelekea Zanzibar kushiriki Mapinduzi Cup huku kukiwa na taarifa ya yanga kujitoa katika michuano hiyo ambapo walipangwa kundi moja, kundi B.

Yanga leo:
1.Yaw Berko, 2.Salum Telela, 3.Stephano Mwasika/Abuu Ubwa, 4.Bakari Mbega, 5.Nadir Haroub Canavaro/Chacha Marwa, 6. Juma Seif Kijiko, 7. Omega Seme/Jerry Tegete, 8. Athuman Idd Chuji/Idrisa Rashid, 9. Pius Kisambale/Hamisi Kiiza, 10. Kenneth Asamoah, 11. Nurdin Bakari.

Azam fc leo:
1. Mwadini, 2.Erasto, 3. Waziri, 4. Aggrey, 5.Moradi, 6. Humud/Suleiman Abubakari, 7. Ngassa/Mcha, 8.Kipre Bolou/Jabir Azizi, 9. Mwaikimba, 10. Abdi Kassim 11. kipre Tchetche/Pazi

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.