Jessca Nangawe
MSHAMBULIAJI mpya wa Azam Gaudence Mwaikimba amesema ushirikiano wa kiuchezaji kati yake na winga Mrisho Ngassa utakuwa moto wa kuotea mbali litakapoanza duru la pili la Ligi Kuu nchini.
Mwaikimba juzi alicheza mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Azam akitoka Moro United dhidi ya timu yake ya zamani Yanga ya jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo ya kirafiki, Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, huku bao moja likipachikwa wavuni na Mwaikimba na lingine likiwekwa kwenye kamba na Ngassa.
"Huu ni mwanzo tu, habari kamili itasomwa mzunguko wa pili wa ligi," alijigamba Mwaikimba wakati akizungumza na gazeti hili.
Mwaikimba alisema amefurahishwa na ushirikiano wa kiuchezaji kati yake na Ngassa na wachezaji wengine kwenye timu hiyo iliyomaliza mzunguko wa kwanza katika nafasi ya tatu ya msimamo.
Ngassa na Tibingana CharlesAlisema furaha yake kubwa ni kuanza kuichezea timu hiyo na kufunga bao, na sasa atakachopigania ni kuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.
"Kila mchezaji anapaswa kucheza, na mimi kama mchezaji (mshambuliaji) jukumu langu ni kufunga mabao, nashukuru nimeanza kazi vizuri," alisema Mwaikimba.
Mwaikimba amemaliza duru la kwanza akiwa na Moro United na kuifungia mabao sita, Mzunguko wa pili unatarajia kuanza rasmi Januari mwakani, ambapo mpaka duru la kwanza linamalizika Simba iko kileleni na pointi 28.
Mabingwa watetezi Yanga ya jijini Dar es Salaam iko katika nafasi ya pili baadaya kuvuna pointi 27, ikifuatiwa na Azam nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23.
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment