Sunday, December 18, 2011

Safari ya Ngassa kujulikana january

Posted By: kj - 11:38 AM

Share

& Comment


Hatima ya mshambuliaji wa Azam FC Mrisho Khalfan Ngassa ya kwenda nchini Marekani itajulikana january mwakani.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyoko kwenye ukurasa wa Azam FC ndani ya Facebook inasema kuwa safari ya Ngassa itajulikana pale dirisha la usajili litakapo funguliwa january mwakani na kwa sasa hawa wezi thibitisha hilo kwani wameahidiwa kurudi Marekani january na hamna makubaliano yoyote yale.

"Habari ya Ngassa itajulikana Januari wakati dirisha la usajili marekani litakapofunguliwa. Kwa sasa tuna ahadi ya kutakiwa kwenda Marekani januari na ahadi hii haijabadilika yaani ipo pale pale lakini kwa kuwa hakuna mkataba baina ya vilabu au klabu na mchezaji nothing can be confirmed for now," ilieleza taarifa hiyo pale alipokuwa anajibu swali kuhusu hatima ya Ngassa.

Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Azam FC akitokea Yanga alikwenda Marekani julai mwaka huu kwa ajili ya kufanya majaribio katika klabu ya Seattle Sounders inayoshiliki ligi kuu ya Marekani 'MLS' ambapo LA Galaxy ndio waliotwa ubingwa huku wakiwa na nyota Robbi Kean na David Beckham.

Ngassa ambaye aliibukia Kagera Sugar baada ya kocha wa Kagera wakati huo Sylvester Mashi kumuona katika timu ya Toto African ya Mwanza, alipata nafasi ya kucheza dhidi ya mabingwa wa Uingeleza Manchester United kwa dakika 15 katika majaribio yake, ambayo inasemakana kila mdau wa klabu hiyo ya Seattle Sounders waliridhika na kiwanga chake.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.