Friday, March 30, 2012

Bocco astaafu Stars

Posted By: kj - 3:22 PM

Share

& Comment


Kinara wa mabao katika historia ya klabu ya Azam FC na kinara wa mabao katika ligi kuu ya Vodacom inayoendelea, John Raphael Bocco 'Adebayor' ameiandikia barua shirikisho la soka nchini TFF ya kustaafu kuichezea timu ya Taifa 'Taifa Stars'. Huku akimuacha njia panda kocha wa kikosi hicho Jan Poulsen.

Bocco amefikia uwamuzi huo kutokana na kuchoshwa na tabia za mashabiki wanao hudhuria mechi za Timu ya Taifa kumzomea kila anapopagwa.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wa Azam FC ndani ya Facebook unasema kuwa Bocco amewaomba TFF walikemee suala la wachezaji kuzomewa wakiwa na jezi ya Taifa.

"John Bocco astaafu kuchezea timu ya taifa na sasa anaelekeza nguvu zake kwa timu yake ya Azam FC, kwa mujibu wa barua yake kwa TFF Bocco amewaomba viongozi wa soka nchini kukemea tabia ya zomea zomea Kama walivyokemea uharibifu wa Mali za uwanja," ili eleza taarifa hiyo.

Katika blog ya Shaffih Sports imemnukuu Bocco akisema; "Nimefikia maamuzi haya baada ya kufikiria sana, nimekuwa nikijitoa kwa hali na mali kulitumikia taifa langu lakini mashabiki wa timu yetu wanaona sifai, hivyo ni bora nijitoe au nistaafu kuichezea timu hiyo ili kuepekana na dhahama zao. Naitakia kila kheri timu yangu ya taifa naipenda na nitaendelea kuipenda siku zote."

Bocco ni miongoni mwa washambuliaji bora nchini kwa kizazi hiki, na amekuwa chaguo la Poulsein toka aachane na washambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa madai ya kwamba hawajitumi wakiwa na timu ya Taifa.

Kama Poulsein akiendelea na uwamuzi wake wakutowajumuisha washambuliaji hao wa TP Mazembe, ni wazi kuwa atakuwa na wakati mgumu katika kusaka washambuliaji watakao ziba mwanya huo.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.