Saturday, March 31, 2012

Mwaikimba asalenda mbio zakiatu cha dhahabu

Posted By: kj - 11:41 AM

Share

& Comment


CALVIN KIWIA

MSHAMBULIAJI wa Azam, Gaudence Mwaikimba amekata tamaa ya kushinda tuzo ya ufungaji bora katika Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2011/12.

Mwaikimba ana mabao sita mpaka sasa kwenye ligi aliyofunga akiwa na Moro United kabla ya kutua Azam kwenye dirisha dogo la usajili msimu huu kwa mkataba wa miezi 12.

Mchezaji huyo ameshindwa kuendeleza makali yake ya kuzifumania nyavu kutokana na kupewa dakika chache za kucheza ndani ya Azam.

Akizungumza na Mwanaspoti jana Ijumaa jijini Dar es Salaam, alisema: "Kwa mtazamo wangu wa haraka nafikiri itakuwa vigumu kuzifikia ndoto za kutwaatuzo ya ufungaji bora kwa msimu huu."

"Ushindani wa namba kwenye kikosi chetu kwa sasa ni mkubwa, nafikiri sina budi kunyoosha mikono kwa hilo," alisisitiza Mwaikimba ambaye aliibuka mfungaji bora kwenye michuano ya Kombe la Taifa mwaka jana baada ya kufunga mabao nane yaliyoufanya Mkoa wa Mbeya kutwaa kombe hilo.

Mshambuliaji huyo amekuwa akipewa dakika 11 za mwisho kukichezea kikosi hicho na kocha Mwingereza Stewart Hall huku mwenzake John Boko akiwa kinara wa ufungaji katika kikosi hicho.

Boko anaongoza kwa ufungaji kwenye Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 15 akifuatiwa na Emmanuel Okwi wa Simba na Kenneth Asamoah wa Yanga wenye mabao 10 kila mmoja.

"Dakika hizi chache hazitoshi tena kuniwezesha kufikia ndoto ambazo nilikuwa nimejiwekea awali, nafikiria kujipanga kwa msimu ujao," alisisitiza Mwaikimba

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.