Shuti la Maganga katika dakika ya 90 na kumshinda mlinda mlango wa Azam FC Deo Munich 'Dida' lilitosha kuwapa point moja Toto African ya Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba na kuendeleza ugumu kwa Azam FC kutoka na point zote 6 katika ukanda huo wa Ziwa.
Katika mchezo huo wa Ligi kuu ya Tanzania Bara, Toto Afrika walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 20 kupitia kwa Mussa Said na dakika 6 mbele Azam walisawazisha goli hilo kupitia kwa Abdulhalim Homoud. Na kupelekea kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.
Kipindi cha pili kilikuwa ni cha kushambuliana kwa zamu lakini Azam FC ndio waliofika katika lango la wapinzani wao mara nyingi na katika dakika ya 83 Azam FC walipata goli la pili kupitia kwa Kipre Tchetche.
Wakati wakazi wa Mwanza wakiwa wameamini kuwa Azam safari hii wamefanikiwa kuchukua point zote 6 katika kanda ya Ziwa, huku wengine wakianza kutoka ndipo Maganga alipo tibua furaha ya Azam kukomba point 6 kwa kuisawazishia Toto katika dakika 90 na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2.
Azam sasa imefikisha point 4 sawa na Mtibwa Sugar ambayo watakutana nayo katika mchezo unaofuata utakaochezwa jumamosi (september 22) katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi Bande jijini Dar es salaam.

0 Maoni:
Post a Comment