Sunday, September 16, 2012

Azam kutua Mwanza leo

Posted By: kj - 1:01 PM

Share

& Comment

Abdulhalim mfungaji wa goli pekee hapo jana

Kikosi cha Azam FC kinatarajiwa kutua Mwanza leo, wakitokea Kagera wakiwa teyari kuwakabili Toto Africa ya Mwanza hapo september 19 katika uwanja wa CCM Kirumba.

Azam FC na Toto African watakutana katika uwanja wa CCM Kirumba jumatano katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara iliyoanza hapo jana kwa Azam kuwachapa goli 1 wakatamiwa wa Kagera.

Kocha msaidizi wa Azam Kali Ongala akizungumza baada ya mchezo wa jana alisema; "Kucheza ugenini mechi ya kwanza huwa ni ngumu, na hasa ukicheza na Kagera Sugar mechi inakuwa ngumu zaidi, nashukuru jitihada za wachezaji zimetupatia ushindi, ni furaha kwetu hii ni mara ya kwanza tunaifunga Kagera kwao".

Kali aliongeza kuwa kujitolea kwa wachezaji wake na kupigana dakika zote za mchezo zimechangia kiasi kikubwa kupatikana kwa ushindi huo ukizingatia timu imecheza katika mazingira tofauti.

Kocha huyo amewataka wachezaji wake waongeze juhudi, wajitume na kujitolea zaidi katika mechi zote ili kufikia matarajio yao.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.