Saturday, September 15, 2012

Azam wavunja mwiko Kaitaba

Posted By: kj - 7:17 PM

Share

& Comment


Mabingwa wa Mapinduzi Azam FC wameanza vyema safari ya kusaka ubingwa wa Tanzania Bara wa msimu wa 2012/13, baada ya kuvunja mwiko wa kutoshinda katika uwanja wa Kaitaba, jioni ya leo.

Goli pekee la kiungo mkabaji Abdulhalim Homoud akiunga mpira wa Erasto Nyoni katika dakika ya 55 lilitosha kuwapatia point tatu muhimu toka kwa Kagera Sugar.

Azam FC kabla ya mchezo wa leo hawakuwahi kuchomoka na ushindi katika uwanja huo unaotumia na Kagera Sugar na hivyo leo kufanikiwa kuvunja mwiko huo.

Azam FC waliuwanza mchezo kwa kasi na kupata kona tatu za haraka kabla ya Kagera Sugar kurejea katika mchezo na kupelekea Azam FC kupunguza mashambulizi na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza.

Katika kipindi cha pili vijana wa Boca walirudi na nguvu mpya na katika dakika ya 55 kupata goli kuongoza kabla ya Kipre Tchetche kupoteza nafasi ya kuipatia Azam FC goli la pili.

Abdulhalim Homoud aliyekuwa na jukumu la kukaba na kuchezesha timu nusura aipatia Azam FC goli la pili baada ya shuti lake kutoka nnje kidogo ya lango katika dakika 58.

Azam FC itashuka tena uwanjani september 19 kuwakabili Toto African ya Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.