Tuesday, September 11, 2012

AZAM WASHINDWA KUTWAA NGAO YA HISANI

Posted By: kj - 6:57 PM

Share

& Comment

Magoli ya John Raphael Bocco 'adebayor' na Kipre Tchetche hakutosha kuwapa ushindi Azam FC hii leo katika uwanja wa Taifa  ukiwa mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Simba SC.

Mchezo huo ulishuhudia Azam FC wakienda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa goli 2-0 yaliyo gungwa na Bocco pamoja Kipre Tchetche, lakini katika kipindi cha pili Simba SC walifanikiwa kurejesha goli zote mbili na kuongeza moja kupitia kwa Daniel Akuffo, Emmanuel Okwi na Mwinyi Kazimoto.

Azam FC watafunguwa mchezo wao wakwanza wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar september 15 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ukifuatiwa na Toto Africans september 19 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. 

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.