Monday, September 10, 2012

SURE BOY KUENDELEA KUWANYANYASA VIUNGO WA SIMBA KESHO?

Posted By: kj - 11:29 PM

Share

& Comment


Ni wakati mwingine wa kiungo anae kuja juu kwa sasa Salum Abubakari 'Sure Boy Jr' kuwazaragaza viungo wa Simba wakiongozwa na Mwinyi Kazimoto katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kesho kwa kiingilio cha Tsh 5000.

Simba na Azam FC wanakutana katika mchezo wa kufungua msimu mpya wa ligi (mchezo wa ngao ya jamii) ambapo kiutamaduni hukutanisha bingwa wa Ligi Kuu na bingwa wa kombe la chama ama shirikisho ambalo linatarajiwa kurejeshwa katika msimu unaofunguliwa kesho.

Kutokana na kukosekana bingwa wa kombe la TFF, mchezo huo unawakutanisha bingwa wa Ligi Kuu dhidi ya mshindi wa pili wa ligi katika msimu uliopita, ambao Simba SC waliibuka bingwa na Azam FC kushika nafasi ya pili.

Michezo kati ya Azam FC na Simba SC huamuliwa na namna viungo wa timu zote mbili zilivyo amka kutokana na timu zote kutegemea eneo la kati kupika magoli yake huku wakicheza soka linalo fanana.

Azam FC inaikabili Simba SC ikiwa na kocha wao mpya ambae alishuhudia kikosi chake kikichapwa goli 3 na kikosi B cha Simba katika michuano BancABC Super8, wakati kocha wa Simba SC akiwa na kumbukumbu ya kufungwa goli 3 toka kwa Azam FC katika mchezo wa robo fainali kombe la Kagame.

Kivutio kingine katika mchezo huo ni Mfumania nyavu wa Azam FC John Raphael Bocco dhidi ya kipa anae daiwa kuwa Tanzania One Juma Kaseja ambapo JB19 amekuwa akiziona nyavu za Kaseja bila ya tatizo lolote na kumfanya awe mshambuliaji pekee wa Tanzania aliyeziona mara nyingi nyavu za Kaseja.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.