Monday, March 25, 2013

AZAM WAANZA KUIVUTIA KASI PRISONS

Posted By: kj - 6:35 PM

Share

& Comment

Kikosi kamili cha wawakilishi pekee watanzania katika michuano ya CAF katika ngazi ya vilabu Azam fc leo wameingia kambini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya Prinsons ya Mbeya.

Azam fc siku ya jumatano ya marchi 27 watakuw wenyeji wa Prinsons katika uwanja wa Azam Complexs uliopo Mbande jijini Dar es salaam, mchezo ambao azam fc watacheza bila ya kocha Stewart Hall ambaye anatumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu.

Hall alifungiwa na TFF michezo mitatu na huo wa jumatano dhidi ya Prisons utakuwa wa pili na adhabu yake kufikia kikomo mwisho mwajuma hili pale azam watakapo wakabili Ruvu Shooting.

Akizungumzia kambi yake iliyoanza leo kocha Stewart Hall amesema kuwa safari hii hana majeruhi yoyote ule baada ya beki Samir Hajji Nuhu kupona jeraha lake lililo muweka nnje ya uwanja kwa takribani wiki nne sasa.

Kambi hiyo ya azam fc itawekwa katika hosteli za timu hiyo zilizopo ndani ya azam complex nnje ya jiji la Dar es salaam Mbande.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.